Sauti Za Usawa
Jamii yenye usawa ina mshikamano na watu wake wana afya, amani na maendeleo.Podcast hii ina lengo la kuchochea usawa wa kweli katika jamii katika nyanja mbalimbali.
Ungana na mwandishi na mtangazaji Aloycea Ngunyali kila mwezi akiibua na kuzungumzia changamoto mbalimbali za kijinsia na jamii.
Atazungumza na wadau, na wanajamii kwa lengo la kuzijadili changamoto hizi na ufumbuzi wake.
Ili kupata maendeleo ya kweli, tunahitaji usawa wa kweli!
Sauti Za Usawa
Latest Episodes
Nani mwenye Jukumu la Malezi Ya Mtoto katika Familia?
Katika familia nyingi, jukumu la malezi bado linaonekana kuwa la mama pekee. Lakini je, huo ndio ukweli? Baba ana nafasi gani katika malezi ya mtoto, na nini hutokea pale jukumu hilo linapoachiwa mzazi mmoja?Katika kipindi hiki tunajadil...
Pengo la kujiamini baina ya wanaume na wanawake
Kwa nini wanaume mara nyingi huonekana kujiamini zaidi kuliko wanawake, hata pale wanapokuwa na uwezo unaofanana? Katika kipindi hiki tunaangazia pengo la kujiamini kati ya wanaume na wanawake, namna jamii inavyolijenga, na athari z...
Mitazamo ya kijinsia kwenye vyombo vya habari na mchango wake katika kuchochea migawanyo na mitazamo ya kijinsia katika jamii.
Katika kipindi hiki , tunaangazia nafasi ya vyombo vya habari katika kuunda na kuendeleza mitazamo ya kijinsia ndani ya jamii. Je, maudhui tunayoyaona kwenye televisheni, redio, filamu na mitandao ya kijamii, na mgawanyo wa majukumu...
Jinsi mitazamo ya kijinsia inavyoathiri utendaji kazi wa wanawake.
Katika kipindi hiki cha podcast, tunajadili jinsi mitazamo ya kijinsia inavyoathiri utendaji kazi wa wanawake katika mazingira mbalimbali ya kazi. Je, matarajio ya jamii, ubaguzi wa kijinsia na majukumu ya kifamilia yanaathiri uwezo...
Jinsi malezi na jamii huathiri mitazamo ya kijinsia katika uchaguzi wa kazi za kitaaluma.
Karibu katika kipindi hiki cha podcast kinachochambua jinsi malezi ya familia na mazingira ya jamii yanavyoathiri mitazamo ya kijinsia katika uchaguzi wa kazi za kitaaluma. Je, bado kuna imani kwamba kuna kazi za wanaume na kazi za ...